MSHAMBULIAJI Robin van Persie amepuuza tetesi kwamba hafurahii maisha chini ya kocha mpya Manchester United, David Moyes.
Taarifa za Daily Star na Metro zilisema
kwamba van Persie amewaambia rafiki zake anamkumbuka kocha wa zamani wa
United, Sir Alex Ferguson, na Mholanzi huyo amesema hashawishiki na
ufundishaji wa Moyes.
Van Persie alifurahia matunda katika
mechi ya kufungua msimu, akifunga mabao mawili katika mechi ya Ngao ya
Jamii dhidi ya Wigan kabla ya kufunga tena mawili katika ushindi wa
United wa 4-1 dhidi ya Swansea.

Mholanzi: Robin van Persie (katikati kushoto) ameshindwa kufunga kwenye Ligi Kuu chini ya kocha mpya, David Moyes

Amepagawa: Mholanzi huyo hakufurahia matokeo dhidi ya Liverpool
Pamoja na hayo, mshambuliaji huyo
alishindwa kufurukuta katika sare ya United ya 0-0 nyumbani dhidi ya
Chelsea kipigo cha 1-0 dhidi ya Liverpool.
Van Persie alionekana kuchanganyikiwa na
hali ya mambo Anfield, na Mholanzi huyo alilimwa kadi ya njano na
angeweza kutolewa nje kwa kadi nyekundu kilaini baada ya kupambana na
Nahodha wa Liverpool, Steven Gerrard.
Lakini Van Persie, aliyefunga mabao 30 United msimu uliopita, amesema anafurahia zama mpya Old Trafford.

Chupuchupu nyekundu: Van Persie alikuwa ana bahati kutoonyeshwa kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu Gerrard (katikati)

Baba: Kuna madai kwamba Van Persie anamkumbuka Ferguson, kocha aliyemnunua United
Aliliambia De Telegraaf: "Ni babu kubwa kufanya kazi na kocha mpya David Moyes. Ninafurahia
mtindo wa Moyes. Anafanyisha mwenyewe mazoezi; yupo karibu na wachezaji
na anatuandaa na kutupa maelekezo vizuri kwa mchezo dhidi ya wapinzani
wafuatao. Ambayo inatuweka vizuri,".
"Kuna hali nzuri ya kufurahisha katika klabu. Taji la mwaka jana limetupa njaa zaidi ya mataji,"alisema.
No comments:
Post a Comment