Thursday 5 September 2013

YANGA WAWAPIGA MKWARA MZITO MBEYA CITY, MWAMBUSI AJIBU MAPIGO, ASISITIZA WAKO VITANI KUPAMBANA NA TIMU ZOTE, SEPTEMBA 14 SOKOINE “NGOMA INOGILE”


MABINGWA watetezi wa ligi kuu soka Tanzania bara, Klabu ya Yanga, wamewafagilia  wanandinga   wao  kwa kutekeleza majukumu yao na ndio maana wanafanya kazi kubwa kuhakikisha wanatetea taji lao walilotwaa msimu uliopita, huku wakimaliza ligi kuu kwa kuwateketeza watani wao wa jadi, Simba SC kwa mabao 2-0.
Afisa habari wa klabu hiyo Baraka Kizuguto amesema kuwa kwa sasa wanaendelea na mazoezi ya kujipanga kuelekea mchezo wa septemba 14 dhidi ya Mbeya City katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.
“Yanga ndio mabingwa watetezi, washindi wa kikombe cha ngao ya jamii, mabingwa watarajiwa wa ligi kuu msimu huu, hivyo kazi ni moja tu, tunapambana na kujipanga kufanya vizuri zaidi, na kikubwa kinachotia moyo ni uwezo mkubwa wa kikosi na morali ya hali ya juu”. Alisema Kizuguto.
IMG_7295 
Mechi iliyopita, Yanga walikabwa na Wagosi wa Kaya na pichani juu, Ally Mustafa ‘ Batez’ golikipa wa Yanga akijaribu kumhadaa nahodha wa Coastal Union, Jerry Santo kabla hajapiga penati katika matokeo ya sare ya  1-1
Kizuguto ameongeza kuwa wanatambua Mbeya City imekuja kwa nguvu sana, lakini kwa Yanga bado sana na lazima cheche zao zitazimwa tu wakiwa nyumbani kwao.
Pia amewataka mashabiki wa Yanga,  nyanda za juu kusini kujitokeze kwa wingi kuwaona mabingwa  watetezi  kwani burudani kubwa itaonekana.
“Yanga ni timu ya wananchi, na kila inapocheza mashabiki wanajitokeza kwa wingi, hivyo tunaendelea kuwaomba wazidi kujipanga kuelekea kipute hicho”. Alijigamba Kizuguto.
DSC_0352 
Kikosi cha Mbeya City kilichotoka suluhu (0-0) na wakali wa Kagera Sugar kutoka Kaitaba katika mechi ya ufunguzi wa ligi kuu soka Tanzania Bara, Agosti 24 Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya


No comments: