Monday 28 April 2014

DUUH! MWALIMU MWENYE ULEMAVU ASHIKILIWA NA POLISI KWAKUDAIWA KUBAKA MWANAFUNZI WA DARASA LA NNE AMBAYE NAYE NI MLEMAVU


Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Ndugu Crispin Meela

 
Na EmanuelMadafa, Mbeya.
MWALIMU Maiko Mwakapala  wa Shule ya msingi Mchanganyiko iliyopo Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya, anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wa darasa la nne ambaye ni mlemavu wa macho.
Mwalimu huyo ambaye naye ni mlemavu wa macho inadaiwa kutenda kosa hilo  April 25 mwaka huu siku ya Ijumaa jioni.
Akizungumza na blog hii  kwa sharti la kutoja jina lake wala picha   mwalimu mkuu wa shule hiyo amekiri kuwepo kwa tukio hilo na kwamba tayari mwalimu Maiko amefikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Amesema, siku ya  Ijumaa jioniApril25 mwaka huu  Mwalimu Maiko alikutwa na mwanafunzi  huyo nyumbani kwake akitaka kumwiingilia kimwili  hivyo walimkamata na kumfikisha kituo cha polisi.
Akizungumzia tukio hilo, Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Chrispin Meela, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba tayari mwalimu huyo amekamatwa.
Aidha, Meela amesema kuwa uchunguzi wa awali aliofanyiwa mwanafunzi huyo umeonyesha kwamba mtoto huyo alikuwa hajaingiliwa kwa siku hiyo lakini amekutwa na magonjwa ya zinaa.
Kwa mujibu wa Meela. amesema mwanafunzi huyo alikiri kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwalimu na kwamba taratibu za kumfanyia vipimo Mwalimu Maiko zinafanyika.
Hata hivyo, Mkuu huyo amesema serikali haitalifumbia macho suala hilo kwani yeye binafsi ambaye pia ni mlezi wa shule hiyo yenye mchanganyiko wa wanafunzi wa kawaida na walemavu atahakikisha hatua za kisheria zinachukuliwa dhidi yake.

No comments: