Monday, 27 April 2015

Kanisa Langu Halitakufa, Anayetaka Kuliangamiza Ataangamia yeye- Gwajima



Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, amesema kuna watu wanaotaka kuua kanisa lake lakini kamwe halitakufa na litang’aa hadi katika kizazi cha mwisho.
 
Akizungumza katika ibada yake iliyofanyika katika Viwanja vya Tanganyika Packers, Dar es Salaam jana, Askofu Gwajima alisema watu hao wamekuwa wakisema kuwa hawalipendi Kanisa la Ufufuo na Uzima na kutaka life.
 
Alisema kanisa lake lina mamlaka na linaungana na sauti ya damu ya mwana kondoo.
 
“Damu ya Yesu ina sauti kubwa ingawaje ilimwagika miaka mingi iliyopita hivyo watu hao wanapaswa kutambua kuwa wanalindwa na Mungu kwa njia ya damu ya Yesu.
 
“Hili ni kanisa la Wakristo wa Agano Jipya wasioogopa mambo ya ajabu ajabu na ya upuuzi puuzi na anayetaka kuliangamiza kanisa hili aangamie mwenyewe na ashindwe kwa damu ya Mwanakondoo,”alisema.
 
Hivi karibuni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe, alitishia kuzifutia usajili taasisi mbalimbali zikiwamo za dini ambazo alisema zinajihusisha kutoa matamko na kushawishi waumini wao kutekeleza matakwa ya siasa.
 
Waziri Chikawe alisema atatumia Sheria ya Vyama vya Jamii Sura ya 337 na kanuni zake zinazosimamia uendeshaji wa taasisi hizo.

No comments: