Waziri Chikawe ameeleza hayo baada ya kupokea taarifa ya ujio wa
wakimbizi na kutembelea kambi ya muda katika uwanja wa lake Tanganyika
mjini Kigoma, ambapo amesema serikali inafuatilia kwa karibu changamoto
zilizojitokeza kufuatia ujio wa wakimbizi, ambapo katibu tawala wa mkoa
wa Kigoma mhandisi John Ndunguru ameeleza kuwa kijiji cha Kagunga sasa
kiko huru baada ya wakimbizi wote kusafirishwa lakini kinakabiliwa na
tatizo la njaa, uharibifu wa mazingira, ugonjwa wa kipindupindu na
uharibifu wa miundombinu.
Kwa upande wake mratibu mkazi umoja wa mataifa nchini Alvaro
Rodriguez ameishukuru serikali ya Tanzania kwa kukubali kuwapokea raia
hao wa Burundi ambao wamekimbia machafuko katika nchi yao na kwamba
jumuia ya kimataifa kwa kushirikiana na mashirika yanayotoa huduma kwa
wakimbizi itaendelea kusaidia ili kuhakikisha wakimbizi na jamii ya
watanzania inakuwa salama.
No comments:
Post a Comment