Akizungumza katika uzinduzi wa programu maalumu ya miaka minne
iliyofanyika wilayani Masasi kata ya Namatutwe kaimu mganga mkuu wa mkoa
Mohamed Kodi amesema katika kata tano za wilaya ya Masasi wanachi 260
walijitokeza kupata huduma hiyo kati yao 112 waligoma kusafishwa macho
jambo ambalo linarudisha nyuma kampeni hiyo ya kutokomeza ugonjwa huo.
Amesema mkoa wa Mtwara unawagonjwa wapatao elfu 36 huku wilaya ya
Masasi ikiwa na wagonjwa wa vikope wapatao elfu tisa hivyo ametaka
wananchi hao kutoa ushirikiano ili kupata tiba hiyo ambayo ni bure.
Hata hivyo baadhi ya wananchi wametaka serikali kutoa elimu kabla
ya kuleta matibabu ili yafanikiwe kuliko ilivyo hivi sasa ambapo
serikali inatumia gharama kubwa kufanikisha kampeni hiyo pasipo
kuelimisha juu ya umuhimu wa tiba hiyo kwa walengwa.
No comments:
Post a Comment