Naibu
waziri wa mawasiliano sayansi na teknolojia Mh Januari Makamba
amewaahidi watanzania kuwa atafumua mfumo mzima wa utawala, serikali na
watumishi wa umma ili kuongeza kasi ya uwajibikaji pamoja na kubana
matumizi kwa kuwa na mawaziri 18 tu.
Mh Makamba ametoa ahadi hiyo jijini Dar es Salaam alipokuwa
anatangaza nia ya kuwania urais ambapo mbali na kuelezea vipaumbele
vyake endapo atapata ridhaa amesema suala la elimu atalipa kipaumbele
kwa kuanzisha mfuko maalum kwa ajili ya kugharamia elimu ya juu.
Kuhusu suala la rushwa Mh Makamba amesema endapo atapata ridhaa
atajenga jamii inayochukia rushwa na kesi zote zitaendeshwa kwa uwazi na
hatakuwa na kigugumizi katika kupambana na rushwa na kwamba viongozi wa
dini wana nafasi kubwa kujenga jamii katika misingi ya maadili mema.
Mh Makamba amesema suala la miundombinu atahakikisha wilaya zote
zinaunganishwa kwa barabara bora na atafufua reli ya Tanga hadi Arusha
ambayo itaunganisha hadi Musoma, na kuhusu ukusanyaji wa kodi serikali
yake itapunguza kiwango cha kodi kwa mwaka kwa mfanyabiashara ndogondogo
ili kupunguza idadi ya wakwepa kodi.
No comments:
Post a Comment