Jeshi
nchini Nigeria linasema kuwa takriban watu 9 wameuawa kwenye
mashambulizi mawili ya kujitoa mhanga kwenye mji ulio kaskazini
mashariki mwa nchi wa Damaturu.
Ripoti zingine zinasema kuwa idadi ya waliokufa ni kubwa.
Mashambulizi mengine yalifanyika kwenye maombi ya kusherehekea siku kuu ya Eid ul Fitr ya kumaliza mwezi mtukufu wa Ramadhan.
Mashambulizi kama hayo hulaumiwa kwa kundi la kiislamu la Boko Haram ambalo limeongeza mashambulizi yake tangu rais Muhammadu Buhari aingie madarakani.

No comments:
Post a Comment