Baada ya tetesi za muda mrefu, hatimaye Mbunge wa Kasulu Mjini (NCCR-Mageuzi ), Moses Machali amejiunga na Chama cha ACT - Wazalendo.
Naibu
Katibu Mkuu wa ACT - Wazalendo, Msafiri Mtemelwa alisema hayo jana
alipokuwa akimtambulisha kwa waandishi wa habari, aliyekuwa Mwenyekiti
wa Kitengo cha Vijana wa NCCR - Mageuzi, Deo Meck ambaye naye amejiunga
na chama hicho.
Machali
ambaye hakuwapo kwenye utambulisho huo, alithibitisha kwa simu jana
kujiunga na chama hicho kipya kinachoongozwa na aliyekuwa Mbunge wa
Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe na kusema atatoa ya moyoni Julai 21 katika
mkutano utakaofanyika kwenye Uwanja wa Kiganamo, Kasulu Mjini.
“Nitakuwa na Zitto na wabunge wengine ambao siwataji kwa sasa,” alisema Machali.
Awali, Mtemelwa alisema Machali amejiunga na chama hicho na kwamba kinachosubiriwa ni utaratibu maalumu wa kumtambulisha kwa wananchi.
Awali, Mtemelwa alisema Machali amejiunga na chama hicho na kwamba kinachosubiriwa ni utaratibu maalumu wa kumtambulisha kwa wananchi.
“Siyo
Machali pekee ambaye amekuwa akihusishwa kuhamia katika chama hiki,
bado kuna wabunge kama wanne, nao wakati wowote watatambulishwa kwa
wananchi. Staili yetu kwa hawa wabunge ni kuwapokea na kuwatambulisha
katika majimbo yao, mbele ya wapigakura,” alisema Mtemelwa.
Alisema
kuhamia katika chama hicho kwa wabunge na vijana wengi kutoka upinzani
ni mwendelezo wake wa kupokea wananchi wa sehemu mbalimbali wanaotaka
demokrasia ya kweli.
Meck
ambaye alikabidhiwa kadi ya uanachama jana hiyohiyo, alisema ameamua
kuhamia ACT kwa sababu vyama alivyopita havikuwa na demokrasia na
mabadiliko ya kweli.
Alisema
baadhi ya vyama vya siasa havijajikita katika kutoa elimu kwa wanachama
wake na kwamba ACT imedhamiria kuirudisha nchi katika misingi
iliyowekwa na waasisi wa Taifa.
“ACT
kipo tofauti na vyama vingine, leo (jana ) nimejiunga na nimepewa
vielelezo ambavyo ni kama mwongozo kwa kile kinachofanywa,” alisema Meck.
Mbali
na mwanachama huyo, pia aliyewahi kuwa mlinzi wa Katibu Mkuu wa Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Khalid Kagenzi naye alionekana
katika ofisi hizo.
Alipoulizwa na waandishi wa habari kama amehamia alijibu: “Ni haki ya kila Mtanzania kujiunga na chama chochote cha siasa anachokitaka. Bado sijachukua kadi yangu ya uanachama,” alisema Kagenzi.

No comments:
Post a Comment