
Majambazi
wanne waliokuwa wamejificha katika ziwa Buligi wilayani Karagwe kwa
lengo la kutekeleza vitendo vya uharifu huku wakiwa na silaha
mbalimbali za kivita wameuwawa na jeshi la polisi mkoani Kagera wakati
wakijiandaa kuvamia na kupora mali za wananchi katika mapambano ya
kujibizana lisasi na jeshi hilo yaliyodumu kwa zaidi ya dakika tano.
Akiongea mara baada ya tukio hilo kamanda wa jeshi la polisi mkoani
Kagera ACP Augastine Leone Ollomi amesema jeshi la polisi lilipata
taarifa kutoka kwa wasamalia wema juu ya ujio wa majambazi hao ambao
walikuwa wamejificha katika ziwa Buligi huku wakijiandaa kwenda kufanya
matukio ya uharifu katika kijiji cha Bisheshe wilayani Karagwe na kwamba
majambazi hao walianza kujibizana risasi na jeshi la polisi na kufaniwa
kuwauwa majambazi wanne na katika tukio hilo hakuna askari yeyote aliye
jeruhiwa.
Kamanda Ollomi ameongeza kwa kusema mkoa wa Kagera sasa unakabiliwa
na matukio mbalimbali ikiwemo mauaji ya watu kukatwa kolomeo na matukio
ya majambazi ambayo yameanza kujirudia ambapo ametoa wito kwa wakazi wa
mkoa wa Kagera kwa ujumla kutoa taarifa kwa jeshi la polisi pindi
wanapoona viashiria vya watu wasio wawema wanaopanga njama za kufanya
matukio ya kiuharifu ili kwapamoja waze kudhibiti matukio hao
yanayojitokeza mara kwa mara katika mkoa huo.
No comments:
Post a Comment