Hali hiyo imejitokeza baada ya mwenyekiti wa mtaa wa Ngazengwa
kudiwa kutokuwa na mawasiliano na watu wa tume ya uchaguzi hali
iliyosababisha aelekeze wananchi kituo kisicho sahhii huku idadi kubwa
ya wananchi wakifika kituoni hapo tangu majira ya alfajiri hadi mchana
bila kukutana na watoa huduma wa BVR na kulalamikia wahusika wa tume
ya uchaguzi kushindwa kutoa vifaa vya kutosha pamoja na mwenyekiti wao
kukwamisha shughuli za zoezi hilo.
Kutokana na hali hiyo, katibu mwenezi wa kata ya mafiga,Sabry Ally
amesema alilazimika kuwatafuta wahusika wa BVR sambamba na mkurugenzi wa
manispaa ya morogoro ili kushughulikia swala hilo na kwamba hatimaye
baadaye zoezi hilo liliendelea kama kawaida.
No comments:
Post a Comment