Mbunge
wa Jimbo la Mbeya Mjini, kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA) Mh. Joseph Mbilinyi aka Mr. Sugu ambaye ni mwana Hip
Hop mkongwe amepata mpinzani aliyetangaza nia ya kuwania kiti hicho
ndani ya chama hicho.
Mpinzani
huyo wa Mh. Sugu ni mwaandishi wa habari ambaye ni mwakilishi wa
kampuni ya magazeti ya Free Media mkoani Mbeya, Christopher Nyenyembe
ambaye amechukua fomu na kusema iwapo atapata ridhaa ya kupeperusha
bendera ya CHADEMA atakuwa jirani na wananchi kusikiliza vipaumbele na
kuahidi kuvitekeleza kwa asilimia 100.
Nyenyembe
aliwahi kuwania nafasi ya Ubunge jimbo la Mbeya mjini katika Uchaguzi
Mkuu mwaka 2010 na kushika nafasi ya tatu kwa tiketi ya CHADEMA,
akitanguliwa na Mh. Sugu.
No comments:
Post a Comment