Tunaelekekea kipindi hiki cha kusherehekea sikukuu ya Eid-El-Fitr na ambapo wananchi wenye imani ya kiislam na hata madhehebu mengine hutumia muda huo kwenda kuabudu pamoja na muendelezo wa sherehe hizo kwenye maeneo mbalimbali ya starehe.
Jeshi la Polisi nchini linatoa wito kwa wananchi wote kuwa makini na kusheherekea sikukuu hiyo kwa amani na utulivu pasipo vitendo ama viashiria vyovyote vya uvunjifu wa amani.
Jeshi
la Polisi nchini linapenda kuwaondoa hofu wananchi kuwa, limejipanga
vizuri kuhakikisha wananchi wanasherehekea sikukuu hiyo kwa amani na
utulivu. Ulinzi umeimarishwa kwenye maeneo yote ya kuabudia, fukwe za
bahari, sehemu za starehe na maeneo mengine yote.
Aidha,
tahadhali zichukuliwe kwa wale wote ambao watakuwa wakitumia barabara
ikiwemo maderera na watembea kwa miguu, kuwa makini kwa kuzingatia
sheria za usalama barabarani na hasa kwa madereva wa magari na pikipiki
kuepuka kwenda mwendo kasi na kutumia vilevi wawapo kazini.
Jeshi
la Polisi linaendelea kuwasisitiza wananchi kutoa taarifa haraka kwenye
vyombo vya dola juu ya kitu chochote ama mienendo ya watu
watakaowatilia shaka mahali popote kwani taarifa hizo za haraka
zitasaidia kuzuia uhalifu kabla haujatokea.
Vilevile
wananchi wachukue tahadhari watokapo kwenye makazi yao, wasiache nyumba
wazi ama bila mtu na endapo italazimika basi ni vema watoe taarifa kwa
majirani zao kwa ajili ya usalama.
TUNAWATAKIA WATANZANIA WOTE SIKUKUU NJEMA YA EID –EL-FITR
Imetolewa na:
Advera John Bulimba-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi
Makao Makuu ya Polisi.
No comments:
Post a Comment