Thursday, 16 July 2015

Vijana 50 ambao ni wanachama wa CCM wajiunga na Chadema.


Siku chache baada ya kumalizika kwa mchakato wa kumpata mgombea wa nafasi ya urais ndani ya CCM, mgawanyiko ndani ya chama hicho umeeanza baada ya uwepo la wimbi kubwa la wanachama kuanza kukihama huku zaidi ya vijana 50 wakijiunga na chama cha Democrasia na maendeleo Chadema.
Sasa ni rasm, Bw Maiko Litanda aliyekuwa kiongozi wa kundi la M4U, lililokuwa likimuunga mkono mbunge wa Monduli Edward Lowasa anasema maamuzi yaliyofanywa kwa manufaa ya wachache ndani ya CCM kwa kumkata jina Bw Edward Lowasa wanasema hawakati tamaa na kwamba safari yao ya matumaini bado inaendelea na sasa inahamia chama cha Democrasia na maendeleo Chadema.
 
Kwa mujibu wa kiongozi huyo wa M4U anasema zaidi ya viajana 100 wamekwisha kujiunga na Chadema ambapo imeshuhudia kad 50 pekee za viajana hao, huku uongozi wa Chadema mkoa ukiwahakikisha kuwafikisha salama katika safari ya matumaini.
 
Katika hatua nyingine chama cha ACT wazalendo kimepokea wanachama 7 kutoka vyama vya upinzani ambapo wanadai kuondoka kwao kunatokana na viongozi wa vyama hivyo kuwa na ombwe la uongozi huku vingine vikiendeshwa kwa ukanda.
 
Vugu vugu hili linakuja siku kadhaa zikiwa zimesalia kabla ya Ukawa kumuweka wazi mgombea wao wa urais huku kukiwa na eti eti huenda mmoja wa vigogo wa CCM yuko mbioni kujiunga na umoja huo.

No comments: