Hizo ni sauti za wafanyakazi hao wakiwa pembeni mwa daraja hilo
wakishikiza kuongezwa fedha huku wakidaia kuwa kwa muda mrefu
wamefanyakazi kwa kunyonywa na sasa imefika mwisho.
Kufuatia hatua hiyo afisa kazi kutoka wizara ya kazi na ajira
alifika katia eneo hilo na kuzungumza na wafanyakazi hao na kubainmisha
mambo mbalimbali ya kisheria lakini wafanya kazi hao wakasisitza kulipwa
kwanza haki zao kabla ya kuendelea na kazi.
Hata hivyo meneja mradi kutoka kampuni inayojenga daraja hilo
kampuni ya REC mhandisi Liu Tao amesema wafanyakazi hao walianza mgomo
wa chini kwa chini tangu mwezi ulipotia na sasa wameamua kufanya mgomo
wawazi wazi laki wameshandaa mpango wa kuwalipa fedha hizo.
Kwa upande wake meneja wa mradi upande wa barabara Bw Jamali Mruma
amesema kwa kiasi kikubwa mgomo utahathiri ukamilikaji wa ujenzi wa
daraja hilo ila jambo kubwa sasa ni kuona nini kifanyike ili kupunguza
ukubwa wa tatizo.
No comments:
Post a Comment