Wednesday 13 January 2016

Naibu Waziri wizara ya fedha aibana TRA Mbeya

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Ashatu Kijaji ameitaka Mamlaka ya Mapato (TRA) mkoa wa Mbeya kuhakikisha inaanda mpango maalumu kwa ajili kudhibiti mapato yanayopotea kutokana na kushamiri kwa biashara ya ubadilishaji wa fedha kiholela katika mpaka wa Tunduma na Zambia.

 Dk. Kijaji ametoa kauli hiyo Mkoani Mbeya baada ya kutembelea TRA mkoani humo na kusema serikali imekuwa ikipoteza mapato mengi hasa kutokana na kuwepo kwa biashara hiyo kiholela.

Amesema serikali lazima ijiendeshe yenyewe kwa kuongeza ukusanyaji wa mapato sanjari na kuzuia mianya yote ya ukwepaji wa kodi pamoja na watu wote kuhakikisha wanalipa

kodi.
Katika hatua nyingine Naibu waziri huyo  ameuagiza uongozi wa TRA katika mpaka wa Tunduma na Zambia kuhakikisha kuwa mizigo yote inayosafirishwa kupitia mpaka huo inafanyiwa tathimini na kulipiwa kwa muda  usiozidi siku moja .

No comments: