Mbunge
wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete amemvaa Naibu waziri wa Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Khamis
Kigwangala na kumwambia anaweza kuwa sehemu ya wachochezi kwa
anachokifanya.
Ridhiwani
Kikwete amebainisha hayo kupitia ukurasa wake wa twitter baada ya Mhe.
Kigwangalla kuonyesha kusikitishwa na kitendo kilichofanywa na
Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma katika kuwafanyia usaili
baadhi ya wataalamu waliojitokeza kwenye usaili wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) ambao umefanyika mapema leo Agosti 30, 2017.
"Unaweza
dhani unauliza swali kumbe nawe unakuwa sehemu ya wachochezi! Mhe.
Waziri unaweza kuwa hujui kusoma lakini picha inatoa jibu sahihi", aliandika Ridhiwani.
Sekretarieti
ya Ajira katika Utumishi wa Umma leo Agosti 30, 2017 ilifanya usaili
kwa ajili ya nafasi za kazi katika Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) ambapo
takribani watu 30,000 walijitokeza huku ikiwa watu 400 pekee ndiyo
wanaotakiwa.
No comments:
Post a Comment