Mbunge
wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya Chama Cha ACT Wazalendo Mh. Zitto Kabwe
amefunguka na kusema kuwa Spika wa Bunge Job Ndugai ameibuka sakata lake
yeye ili kutaka kufunika nguvu ya wananchi kuhoji juu ya kupigwa risasi
Mbunge Tundu Lissu.
Zitto
Kabwe amesema hayo leo mara tu baada ya Spika wa Bunge Job Ndugai leo
bungeni kusema anauwezo wa kumzuia Mbunge huyo asizungumze bungeni hadi
mwisho wa bunge hilo kwani Zitto hawezi kupambana naye.
"Nimegundua
Spika Ndugai ameibua mashtaka yangu ili kufunika ufuatiliaji wa
wananchi kuhusu Tundu Lissu kupigwa risasi. Nimeamua sitawapa hilo"
aliandika Zitto Kabwe kupitia mtandao wake wa Twitter
Spika
wa Bunge Mhe. Job Ndugai jana aliagiza Mbunge Zitto Kabwe pamoja na
Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea kufika kwenye Kamati ya Haki, Maadili na
Madaraka ya Bunge ili kuhojiwa kutokana na kauli walizotoa hivi
karibuni, jambo ambalo Zitto Kabwe anadai limeibuliwa kwa lengo la
kupunguza nguvu ya wananchi kutohoji sakata la Tundu Lissu kupigwa
risasi.
No comments:
Post a Comment