MAHENGE&FAMILY COMPANY LTD
Ni watunzaji wa
mazingira na wapandaji wa miti katika
mkoa wa Mbeya wilaya Rungwe na ndio washindi wa tunzo ya Raisi kwa mwaka 2012.pia mahenge &family company
ltd wana jishughuliha na utengenezaji wa mizinga ya nyuki wa asili na utegaji
wa mizinga hiyo,mpaka kufikia mwezi huu wana mizinga 280 ambayo imetegwa katika
misitu mbalimbali katika kijiji cha ngumbulu.hivyo kwa kufanya hivyo kampuni
imetoa ajira kwa vijana wengi wanao zunguka eneo la mradi misitu,kampuni pia
imetoa miche zaidi ya elfu kumi kwa vijana hao.
KAZI ZINAZOFANYWA NA KAMPUNI
.Kuotesha miche ya miti
.Kupanda miti kwenye mashamba ya kampuni
.Kushauri na kufundisha watu wengine upandaji wa miti
.kushauri watu wasiuze mashamba na badala yake wapande miti
.kushauri watu kuto hamia mjini na badala yake waendelee
kufanya kazi vijijini ambazo zitawongezea vipato
.kufundisha vijana ujasiliamali.kama vile,udereva,kupasua
mbao, kukata miti kwa kutumia mashine,kuendesha pikipiki,kulima mazao
mbalimbali.
JINSI WANAKIJIJI WANAVYO NUFAIKA NA MRADI
.Kutoa ajira
.Wanakijiji wana pata kuni,fito,mabanzi na mbao kutoka
katika mradi wa msitu
.kampuni huwa saidia wanakijiji wakati wa matatizo
mbalimbali kama vile kubeba wagonjwa na maiti
kwa gari ya kampuni
.kampuni ilitoa
vitabu katika shule ya msingi ngumbulu vyenye thamani ya shilingi laki tisa na
nusu.
.kampuni huji husisha na marekebisho mbalimbali ya
miundombinu ya balabala pindi inapo haribika
.Pia kampuni hujihusisha na udhamini wa michezo
mbalimbali,kwa kutoa jezi na mipira
Pia kampuni hii ni miongoni mwa wanabodi wa kutengeneza
sheria zitakazo tumika katika nchi yetu kwa masuala ya muungano wa misitu ya
watu binafsi na serikali.
Ambayo ni PUBLIC PRIVATE PARTNERSHIP[PPP]
Hivyo tunawashauri vijana waishio mijini kuacha kufanya kazi
za mda mfupi [yaani kutafuta pesa asubuhi na kutumia zote jioni] Naomba
tubadilike na tukumbuke kujiwekea hazina.wenye mashamba vijijini turudi
tukapande miti.
No comments:
Post a Comment