Wednesday, 13 September 2017

BOSI WA ZAMANI WA ATCL, DAVID MATAKA NA MWENZAKE WAHUKUMIWA KULIPA FAINI YA MIL 70 AU KIFUNGO CHA MIAKA SITA JELA

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu aliyekuwa Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), David Mataka na mwenzake Elisaph Mathew, aliyekuwa Kaimu Afisa Mkuu kitengo cha fedha cha ATCL kulipa faini ya jumla ya sh. Milioni 70 ama kutumikia kifungo cha miaka sita jela. Pia mahakama imewaamuru kulipa hasara waliyoisababishia ATCL katika ununuzi wa magari chakavu 26 ambayo in USD 143,442.75.

Pia Mahakama imemuachia huru William Haji ambaye alikuwa ni Mkaguzi Mkuu wa hesabu za ndani za ATCL.
 
CREDIT ;MICHUZI

No comments: