Saturday 19 November 2016

WADAU WA ELIMU WILAYANI KYELA WATAKIWA KUCHANGIA UJENZI WA MADARASA

Diwani wa kata ya Nkuyu wilayani Kyela, Kain Alexander mwakanyemba kupitia Chadema, amewataka wadau wa Elimu wilayani humo kujitokeza kusaidia ujenzi wa shule ya msingi Nkuyu.

Akizungumza na mtandao huu shuleni hapo, Mwakanyemba alisema, wadau wanatakiwa kujitokeza ili kusaidia ujenzi wa miundombinu ya madarasa.

"Tumejitahidi kufanya ujenzi wa madarasa mawili ambayo ndiyo tunamalizia kuchapia, ila kuna madarasa mengine miwili yanatakiwa kufanyiwa marekebisho " alisema.

Pia amewashukuru Meya wa ilala Charles Kwiyeko aliyesaidia kiasi cha shilingi milioni moja kwaajili ya ujenzi wa shule, vile vile Naibu spika Tulia Mwansasu aliyetoa kiasi cha laki tano.

No comments: