Thursday, 11 May 2017

Waziri Mkuu aeleza hali ya sukari nchini kuelekea mwezi wa Ramadhan

Mbunge Jakuh Hashim Ayoub amemuuliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuhusu mwezi mtukufu wa Ramadhan na kuna tatizo la sukari huku wananchi wakiwa na uhitaji na kwamba hivi sasa zipo tani 100,000.

Amemweleza Majaliwa kuwa sukari iliyoagizwa kwa watu waliopewa vibali vya sukari itakuwa imekwisha wakati mwezi mtukufu wa Ramadhan utakapoanza.

Akijibu swali hilo Majaliwa amesema kuhusu kupungua kwa sukari na mahitaji yake nchini kuwa Serikali iko macho na itafanya jitihada za kupata mahitaji yote.

“Mahitaji ya sukari nchini ni tani 420,000 lakini kwa sasa tunazalisha tani 320,000 hivyo mwaka huu Serikali imeagiza tani 80,000 na tayari tani 35,000 zimeshaingizwa nchini,”amesema Majaliwa.

Hata hivyo, Majaliwa amewasihi wafanyabiashara kushusha bei ya sukari waliyoipandisha kwani Serikali inashirikiana nao ili kuweza kuweka mazingira rafiki kwa wananchi.

No comments: