Thursday 1 June 2017

NAHODHA WA EVERTON ALIYELETWA NA SPORTPESA AJICHANGANYA NA VIJANA WA BONGO

Leon ameongoza na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Everton, Robert Elstone ambaye kitaaluma ni mhasibu.

Wawili hao wakiwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam walipata nafasi ya kuona baadhi ya wachezaji wenye vipaji ambao walipata nafasi ya kuonyesha vipaji vyao kwa muda mfupi.

Nahodha huyo pia alipata nafasi ya kupiga danadana kwa muda mfupi na wachezaji hao wa Tanzania ambao ni taifa la baadaye.

Kati ya watu waliokuwepo uwanjani ni mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe. Pia Ofisa Mtendaji Mkuu wa SportPesa Tanzania, Pavel Slavkov.

Osman aliichezea Everton katika maisha yake yote ya soka kuanzia mwaka 2000 hadi 2016 japokuwa hapo kati wakati anaanza kukomaa alitolewa kwa mkopo kwenda Carlisle United na Derby County.

No comments: