Maelfu
ya raia wa Ugirik usiku wa leo wametawanyika katika mitaa ya mjini
Anthens karibu na jengo la bunge, wakifurahia kura ya hapana
waliyoipiga ambayo imeshinda kwa ya asilimia 60.
Tsipras ameongeza kuwa serikali ya Ugiriki iliitisha kura hiyo ya maoni ikiamini kuwa kura ya Hapana italeta makubaliano mazuri, pamoja na kwamba kuna onyo kutoka kwa viongozi wa ukanda wa Euro kuwa hatua hiyo itasababisha Ugiriki kuondolewa katika nchi wananchama wa ukanda huo.
Naye Rais wa Bunge la Jumuiya ya Ulaya Martin Schulz amesema kuwa kura hiyo ya HAPANA inaiacha Ugiriki katika mazingira mabaya zaidi kuhusiana na mzozo wa madeni na vikwazo vya kimataifa.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier anasema kwa matokeo hayo sasa umamuzi ni wa mahakama ya Ugiriki kwani wapiga kura wamepinga kwa nguvu zote masharti ya wakopeshaji wa kimataifa
Matokeo haya yanasababisha kukubalika zaidi kwa Waziri mkuu wa Ugirik Alexis Tsipras japo kuwa pia anakuwa na wajibu mkubwa wa kukabiliana na mazingira yote ya kipindi hiki cha mpito kuhusiana na mzozo wa madeni.
No comments:
Post a Comment