Rais
John Magufuli ameagiza Sh200 milioni zilizopangwa kutumika katika mradi
wa maji katika kambi ya jeshi zianze kuimarisha miradi ya maji kwa
wananchi kwanza.
Akizungumza
leo, Alhamisi Julai 20 katika ziara yake akiwa ameambatana na Rais wa
Burundi, Pierre Nkurunzinza, Magufuli amesema amebaini kuwa pampu za
maji wilayani Ngara zimeharibika kwa zaidi ya wiki tatu na kuwa wilaya
hiyo ina uhaba mkubwa wa maji.
Alimuita, Mhandisi wa Maji ajieleze ni kwa nini pampu hizo hazifanyi kazi na baada ya kumsikiliza ndipo alipofanya uamuzi huo.
Akifafanua
kuhusu hali ya maji, mhandisi huyo amesema awali visima vya maji
wilayani hapo vilikuwa vikihudumia watu 400 lakini kwa sasa wilaya hiyo
ina watu zaidi ya 240,000 na hivyo visima hivyo havitoshelezi.
“Tulikuwa
tuna idadi ndogo ya watu sasa hivi imeongezeka, lakini tangu pampu
iharibike, tumetengeneza mbili na kisima kimoja hakina pampu,” amesema.
Baada
ya mhandisi huyo kufafanua hayo ndipo Rais alimuita Mkurugenzi wa
Halmashauri kueleza mipango yake, ndipo Mkurugenzi huyo aliposema mradi
wa maji wa Sh200 milioni utaanza kwanza katika kambi ya jeshi.
Kauli hiyo ndiyo iliyomfanya Rais Magufuli kushauri fedha hizo zitumike katika miradi ya maji katika makazi ya wananchi kwanza.
“Wanajeshi wapo 200 na wananchi wapo zaidi ya 20,000 sasa si bora waanze wananchi kwanza,” amesema.
No comments:
Post a Comment