Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Kazi,Ajira, Vijana
na Watu wenye Ulemavu, ametoa siku 30 kwa waajiri wote nchini ambao
hawajasajili, kujisajili katika mfuko wa fidia kwa wafanyakazi (WCF) na
kutoa michango kwa wakati.
Mh.
Mhagama ametoa agizo hilo leo jijini Mbeya wakati wa ukaguzi wa
kushtukiza jijini humo na kuwabaini waajiri ambao bado hawajatekeleza
Sheria ya fidia kwa Wafanyakazi Sura 263 Marejeo ya Mwaka 2015 kifungu
cha 5, ambayo inawataka waajiri wote kutoka sekta ya Umma na binafsi
Tanzania Bara kujisajili kwenye mfuko huo.
Mhagama
amefafanua kwamba, mwajiri ambaye hajajisajili kwenye mfuko, anaweza
kufikishwa mahakamani na adhabu ni pamoja na kutozwa faini ya kiasi cha
fedha kisichozidi shilingi milioni 50 au kifungo kisichozidi miaka 5
jela au vyote kwa pamoja,
Katika
ziara hiyo ya ukaguzi wa kushtukiza Mh. Mhagama alifuatana na
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini wa Mfuko wa fidia kwa
wafanyakazi, Dk. Abdulsalaam Omar, na aliikagua hospitali ya K’s iliyoko
eneo la Mafyati na Shule ya Sekondari ya Saint Aggrey iliyoko Uyole na
kubaini kuwa taasisi hizo hazijajisajili katika mfuko.
No comments:
Post a Comment