Waangalizi
wa kimataifa wa Umoja wa Afrika na Jumuiya ya Madola wametoa ripoti yao
ya awali kuhusu uchaguzi Kenya na mazungumzo yao na kambi ya upinzani
ya National Super Alliance (Nasa) waliowasilisha madai kwamba kompyuta
za IEBC zimeingiliwa na upande Jubilee kuvuruga matokeo halisi ya kura.
Kiongozi
wa ujumbe wa Waangalizi wa Umoja wa Afrika, Thabo Mbeki alisema ni
kweli mgombea wa Nasa, Raila Odinga na ujumbe walikutana nao wakiwa na
nyaraka za madai kuhusiana na Jubilee walivyovamia kompyuta hizo.
Mbeki
alisema waliwasikiliza na kuwaeleza kuwa watalifikisha suala hilo IEBC.
Hata hivyo alisema Nasa walitaka waangalizi hao wafanyanyie kazi
nyaraka hizo kwa kuchunguza.
"Kwa
mtu kama sina utaalamu wa teknolojia kuniambia nichunguze ni sawa na
kuniambia nifanye kazi ambayo sina ujuzi," alisema Mbeki.
Alisema
kazi ya waangalizi ni kuangalia ni si kuchunguza, kwa kuwa wao jukumu
lao ni kuangalia namna mchakato mzima ulivyofanyika kama ulifuata sheria
za nchi husika na taratibu za kuheshimu demokrasia walizojiwekea katika
Umoja wa Afrika.
Alisema tuhuma zote zilizotolewa na Nasa wameziwasilisha kwa mamlaka husika ndani ya Kenya.
Kwa
upande wake mkuu wa ujumbe wa waangalizi wa Jumuiya ya Madola, Rais wa
zamani wa Ghana, John Dramani Mahama alisema walikutana na Odinga na
ujumbe wake na walitoa madai ya kompyuta za IEBC kuvamia huku wakiwa na
nyaraka kama ushahidi wa madai yao, hata hivyo Mahama alisema nao
waliwaeleza kwanza hawana utaalamu wa teknolojia hiyo, lakini jukumu lao
ni kuangalia kama utaratibu mzima wa uchaguzi umefuata sheria na katiba
ya nchi na madai mengine ya ukiukwaji wa taratibu yana utaratibu wake
uliowekwa kwa mujibu wa sheria.
Chanzo: Mwananchi
No comments:
Post a Comment