Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles John Mwijage amekiri kupokea
wito wa kwenda nchini India kwa ajili ya kusafisha jina la Tanzani
baada ya watu wanaodaiwa ni madalali tapeli wa zao korosho kulichafua.
Mh.
Mwijage ameyasema hayo jana ambapo amedai kuwa anaoushahidi kuwa
kampuni hizo za udalali zilichafua jina la nchi hivyo ni lazima
awafikishe katika mikono yua sheria.
“Vitendo
hivi vinavyofanywa na makampuni haya havivumiliki kwani mchezo huu ni
mauti kwetu na nitahakikisha wanachukuliwa hatua kwani ninao ushahidi
unaotosheleza,”alisema Mwijage.
Mh.
Mwijage amefafanua kwa kusema kwamba watu wametapeliwa kwa kuambiwa
pindi wanapoagiza mazao watoe pesa ya kianzio ambayo ni kuanzia dola za
Marekani 123,000, sawa na Sh275 milioni na dola 200,000 sawa na
Sh448milioni za kitanzania.
“Nimepokea
wito kutoka India kwa ajili ya kwenda kusafisha jina la nchi kutokana
na taswira iliyosababishwa na uwepo wa matapeli hao,”alisema Mwijage.
No comments:
Post a Comment