Rais John Pombe Magufuli amefunguka na kutoa kauli yake kuhusu baadhi ya
wafungwa ambao wamehukumiwa kunyongwa kutokana na makosa mbalimbali na
kudai kuwa yeye anaogopa kusaini ili wafungwa hao wanyongwe.
Rais Magufuli amesema hayo leo Ikulu jijini Dar es Salaama wakati
akimuapisha Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma na kusema
anatambua kuwa idadi wa wafungwa waliohukumiwa kunyongwa ni wengi sasa
ila anaomba asipewe hiyo orodha.
"Sisi wanasiasa tunaogopa kunyonga, natambua kuwa sasa orodha ya watu
ambao wanatakiwa kunyongwa ni kubwa sana ila mimi naomba hiyo orodha
msiniletee kwa sababu najua ugumu wake ulivyo" alisisitiza Rais Magufuli
Mbali na hilo Rais Magufuli amesema kuwa amechukua muda mrefu kumteua
Jaji Mkuu wa Tanzania kutokana na ukweli kwamba alikuwa anatafuta mtu
ambaye anaweza kuendana na dhamira yake ya kupambana na rushwa hivyo
alipojilidhisha na jaji huyo ndiyo maana ameamua kumteua kuwa Jaji Mkuu
wa Tanzania.
No comments:
Post a Comment