Monday, 11 September 2017

Kikwete Afunguka Mazito Sakata la Tundu Lissu


SeeBait
Mbunge wa Jimbo la Chalinze (CCM) Mhe. Ridhiwani Kikwete amefunguka na kuwataka wananchi na baadhi ya viongozi wakae kimya kama jambo hawalifahamu undani wake kwani kufanya hivyo hakutaweza kusaidia upelelezi.
 
Ridhiwani Kikwete amebainisha hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram baada ya baadhi ya viongozi kujaribu kutumia tukio lililompata Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu kupigwa risasi na watu wasiofahamika kama jukwaa la kisiasa kwa kutaja wahusika wa jambo hilo bila ya kuwa na ushahidi wa aina yeyote ile mbapo ni hatari kwa usalama wa nchi.

"Kama jambo haulijui, haujalishiriki bora unyamaze. Kutunga uongo au kuandika sana ili uonekane unajua kufikiri dhidi ya uhalisia hakutasaidia upelelezi wala haki kuonekana ikitokea. Tuwe watulivu katika kipindi hiki ili haki itendeke", amesema Ridhiwani Kikwete.

No comments: