Mbunge
wa Jimbo la Chalinze (CCM) Mhe. Ridhiwani Kikwete amefunguka na
kuwataka wananchi na baadhi ya viongozi wakae kimya kama jambo
hawalifahamu undani wake kwani kufanya hivyo hakutaweza kusaidia
upelelezi.
Ridhiwani
Kikwete amebainisha hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram baada ya
baadhi ya viongozi kujaribu kutumia tukio lililompata Mbunge wa Singida
Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu kupigwa risasi na watu wasiofahamika
kama jukwaa la kisiasa kwa kutaja wahusika wa jambo hilo bila ya kuwa na
ushahidi wa aina yeyote ile mbapo ni hatari kwa usalama wa nchi.
"Kama
jambo haulijui, haujalishiriki bora unyamaze. Kutunga uongo au kuandika
sana ili uonekane unajua kufikiri dhidi ya uhalisia hakutasaidia
upelelezi wala haki kuonekana ikitokea. Tuwe watulivu katika kipindi
hiki ili haki itendeke", amesema Ridhiwani Kikwete.
No comments:
Post a Comment