Spika
wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amefunguka na kudai atahakikisha yeye
na wabunge wanampa ushirikiano Jaji Mkuu Prof. Ibrahim Hamis Juma
aliyeapishwa leo baada ya kuteuliwa siku ya jana Septemba 10 mwaka huu.
Ndugai
ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa anatoa salamu za wabunge katika
ghafla hiyo ya uapisho iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar
es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa bila ya
kumsahau Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
"Sisi
kama bunge tunawahakikishia ushirikiano mkubwa sana kwa kuhakikisha
kazi za Mahakama zinaendelea kama zilivyo kikatiba na tutaheshimu sana.
Yale maneno na makombora moja moja ya bungeni ni vitu vya kawaida, ndiyo
utamaduni wa bunge",amesema Ndugai.
Aidha,
Ndugai amesema Mahakama inamchango mkubwa kwa wananchi pamoja na taifa
kwa ujumla kwa kuwa hicho ndicho chombo pekee kinachoweza kumtetea
mnyonge kuweza kupata haki yake kutoka kwa waporaji.
"Kuwepo
kwa Mahakama ndiyo usalama wetu, amani, kheri na matumaini ya mnyonge
katika sheria na maamuzi ya Mahakama. Kwa hiyo tunakutakia kila la kheri
katika kazi yako, tunakuombea kwa Mwenyezi Mungu na tutakusaidia na
kuomba msaada wako",amesisitiza Ndugai.
Kwa
upande mwingine, Jaji Mkuu Prof. Ibrahim Hamis Juma ameahidi kufanya
kazi katika maadili ya kisheria pamoja na kurudisha imani ya wananchi
kuhusiana na kupata misaada ya kisheria inayotolewa katika Mahakama
mbalimbali ndani ya Tanzania
No comments:
Post a Comment