Katibu
Mkuu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji amesema hawezi kwenda kuripoti
Polisi kama alivyotakiwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles
Muroto kwa kuwa hakuambiwa siku maalumu ya kwenda.
Kamanda
Muroto amemtaka Dk Mashinji afike ofisi ya Upelelezi wa Makosa ya jinai
mkoani Dodoma au ofisi kama hiyo iliyopo Kituo cha Kikuu cha Polisi
Kanda Maalumu ya Dar es Salaam ili kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo
kuhusu tukio la kushambuliwa kwa risasi Mbunge wa Singida Mashariki,
Tundu Lissu.
“Nina
taarifa za kuitwa Polisi, lakini haziko ‘specific’. Ni wakati wowote
naweza kwenda? na hawajasema nikaripoti wapi. Kwa hiyo, wakinihitaji
watakuja kuniambia,” amesema Dk Mashinji
Lissu alipigwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7 mchana alipokuwa akielekea nyumbani kwake Area D mjini Dodoma.
Kwa sasa Lissu anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Aga Khan jijini Nairobi, Kenya.
No comments:
Post a Comment