Wabunge wa CUF wameonekana kuvurugana bungeni kutokana na mgogoro unaoendelea katika chama hicho.
Mvurugano
huo umeonekana leo Jumatatu mjini Dodoma baada ya wabunge wanaomuunga
mkono Profesa Ibrahim Lipumba ambaye ni Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa
na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kufanya uchaguzi na kumchagua
Mbunge wa Mtwara Mjini, Maftaha Nachuma kuwa mwenyekiti wao bungeni.
Naibu
Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson ametangaza kuwa Spika wa Bunge, Job
Ndugai amepokea barua kutoka kwa Katibu wa CUF, Magdalena Sakaya kuhusu
safu hiyo ya uongozi.
Baada
ya tangazo hilo, Mbunge wa Malindi, Ally Salehe aliomba mwongozo wa
Spika akitaka kujua ni nani anaamua kuhusu uongozi wa wabunge bungeni
kwa sababu wao wameshafanya uchaguzi na kumchagua Mbunge wa Temeke,
Abdallah Mtolea kuwa mwenyekiti wao baada ya kufukuzwa kwa wabunge
wanane.
Pia, amehoji inawezekanaje kuwa na viongozi wawili bila wa kwanza kufutwa.
Akijibu
mwongozo huo, Dk Tulia amesema Spika amepokea taarifa ya viongozi hao
lakini hajapokea taarifa ya uchaguzi wa upande wa akina Ally Salehe
ambao unamuunga mkono Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad.
Amesema watakapopeleka taarifa yao ndipo Spika ataamua.
Chanzo: Mwananchi
No comments:
Post a Comment