Watoto
wa kike elfu tatu, mia tatu ishirini na tisa kati ya watoto elfu tano
mia sita sitini na wawili waliopangiwa kukeketwa katika msimu wa
ukeketaji wa mwaka 2016 katika wilaya ya Serengeti mkoani
Mara,waliokolewa kufanyiwa ukatili huo baada ya Kanisa la Anglikana
doyosisi ya Mara kujenga kituo maalum cha kuwahifadhi baada ya kukataa
kukeketwa na kuzikimbia familia zao.
Akizungumza
wakati wa kikao cha Bodi ya kituo hicho kinachojulikana kama Nyumba
Salama, Meneja wa Shirika la Utafiti na Tiba Barani Afrika-AMREF wilaya
ya Serengeti Bwana GODFREY MATUMU amesema utafiti uliofanywa wilayani
humo umebaini kuwa katika msimu huo wa ukeketaji, baadhi ya wazazi
waliwakeketa watoto elfu mbili, mia tatu thelathini na watatu nyakati za
usiku na wengine walifanyiwa ukatili huo baada ya kufichwa katika
wilaya ya Tarime na nchi jirani ya Kenya.
Hata
hivyo, pamoja na mafanikio hayo ya Nyumba Salama ya kuwakoa watoto wa
kike na vitendo hivyo vya ukatili dhidi ya ukeketaji, mgogoro mkubwa wa
uendeshaji wa kituo hicho umeibuka,hali ambayo imesababisha Askofu wa
Kanisa la Anglikana dayosisi ya Mara Dakta GEORGE OKOTH kuwafukuza kazi
baadhi ya walikuwawatumishi wa kituo hicho.
Chanzo: ITV Tanzania
No comments:
Post a Comment