Wednesday 25 October 2017

Jaji amtaka Rais kufika mahakamani kujibu kesi inayomkabili

Jaji wa Mahakama Kuu imeamuru rais wa zamani wa Nigeria Goodluck Jonathan apewe hati ya kuitwa mahakamani kuhusu kesi ya rushwa inayomkabili msemaji wake wa zamani katika chama cha Peoples Democratic Party (PDP).

Hati ya kuitwa mahakamani ni hatua ya kushangaza na itafuatiliwa kwa karibu kutokana na ukweli kwamba Jonathan amekuwa akitajwa katika matukio mengi ya kifisadi japokuwa hakuwahi kuitwa na kuhojiwa rasmi.

Suala kama atafika mahakamani au la itategemea ikiwa ni lini na ikiwa atapelekewa rasmi hati ya mahakamana.

Msemaji wa zamani wa Jonathan, Olisa Metuh anakabiliwa na kesi anayoshtakiwa kwa kosa la kujipatia kwa njia za udanganyidui dola 1.1 milioni za Marakeni kutoka kwa Sambo Dasuki mshauri wa masuala ya usalama wa Jonathan.

Katika utetezi wake, msemaji huyo ameng’ang’ania kwamba alipokea fedha hizo kwa maelekezo yaliyotolewa na Jonathan ili kugharimia kampeni za kutetea kiti chake mwaka 2015.

Jumatatu, mawakili wa Metuh walisema kwamba wanakusudia kumwita rais huyo wa zamani kama shahidi.

Jaji wa Mahakama Kuu ya Shirikisho Abang Okon anayesikiliza shauri hilo alisema itakuwa “sawa na ukiukwaji wa haki zake (Metuh) kwa usikilizwaji wa haki ikiwa hatatia saini hati ya kuitwa mahakamani".

"Sina chaguo jingine zaidi ya kutia saini hati ya mahakama ya kumlazimisha rais wa zamani Goodluck Jonathan kufika mahakamani jana Oktoba 25, 2017 ili aweze kutoa ushahidi wake," aliongeza.

No comments: