Wednesday 25 October 2017

Nassari Amuonya RC Gambo


SeeBait
Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari ametoa onyo kwa viongozi wa Serikali ya Arusha, akiwepo Mkuu wa Mkoa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru kwamba waache kuwatishia wagombea wa chama chake (CHADEMA) ikiwepo kuwashawishi waajiondoe kwenye uchaguzi wa madiwani unaotarajiwa kufanyika Oktoba 26.

Mh. Nassari amewaonya viongozi hao huku akiwakumbusha kwamba wanatakiwa wafahamu wana-deal na watu wa aina gani huku akiwakumbusha kwamba kama wanataka kurekodiwa.

"Onyo kwa RC na DC! acheni kuwatisha wagombea wetu, acheni kuwatuma watu wakiwemo viongozi wa dini kuwashawishi wajiondoe kwa ahadi zilezile. Mmesahau mna-deal na watu wa aina gani?? Au bado mnataka kurekodiwa??" Ameandika Nassari katika mtandao wake wa Facebook.

Ameongeza kwamba "We are determined, (Tumedhamiria)  Tukutane kwa debe!!"

Mapema mwezi huu Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ilitangaza kwamba  uchaguzi mdogo wa marudio wa madiwani katika kata 43  utafanyika Novemba 26 mwaka huu, huku Arusha ikiwa imepoteza kata kumi.

No comments: