JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
Ofisi ya Kamanda wa Polisi,
Mkoa wa
Mbeya,
Namba ya simu 2502572
S. L. P. 260,
Fax - +255252503734
MBEYA.
E-mail:- rpc.mbeya@tpf.go.tz
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 23.10.2017.
Jeshi
la Polisi Mkoa wa Mbeya limeendelea kufanya misako, operesheni na doria zenye
tija katika maeneo mbalimbali ili kudhibiti uhalifu na wahalifu na limekuwa likishirikiana
na wananchi na wadau wengine katika jitihada hizo za kukabiliana na uhalifu na
wahalifu na kupata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kupungua kwa matukio
makubwa ya uhalifu.
Mafanikio
yaliyopatikana katika Misako/Doria ni kama ifuatavyo:-
KUPATIKANA NA NOTI BANDIA.
Mnamo tarehe 22.10.2017 majira ya saa
15:00 Alasiri, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilifanya msako huko eneo la
Sisimba lililopo Kata na Tarafa ya Sisimba, Jiji na Mkoa wa Mbeya na kufanikiwa kumkamata mtu mmoja
aliyefahamika kwa jina la FAUSTINA
MAGANGA [20] Mkazi wa Mtaa wa Teku akiwa na noti bandia 10 za Tshs 10,000/=
sawa na Tshs 200,000/= kama zingekuwa halali.
Noti
hizo zilikuwa na namba BU 3352850 noti 5 na BU 3352846 noti 5. Mtuhumiwa
atafikishwa Mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaongeza
jitihada za kuzuia na kupunguza matukio ya ajali za barabarani kwa kuhakikisha madereva
na watumiaji wengine wa barabara wanafuata sheria na alama za usalama
Barabarani. Aidha kumekuwa na ajali 01 ya vifo na majeruhi kama ifuatavyo:-
Mnamo tarehe 22.10.2017 majira ya saa
15:45 jioni huko maeneo ya DM Hotel, Kata ya Bulyaga, Tarafa ya Tukuyu
mjini, Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya katika Barabara kuu ya Tukuyu/Mbeya, Gari
yenye namba za usajili T 756 BGS aina
ya Toyota Chaser iliyokua ikiendeshwa na dereva aitwaye CHARLES MWAMBENA [26] Mkazi wa Tukuyu ikitokea Kitongoji cha
Bagamoyo kuelekea Tukuyu mjini iliacha njia na kwenda kuwagonga watembea kwa
miguu wawili 1. BENARD FORTNATUS KASELA [22] Mwanachuo wa FDC – Katumba na Mkazi wa
Nansio - Ukerewe
na
2. AYOUB WILLIAM MWAIJENGO
[20] Mwanachuo wa FDC – Katumba, Mkazi wa mbeya na kusababisha vifo vyao wakiwa
wanapatiwa matibabu katika Hospitali ya Wilaya – Makandana.
Inadaiwa
kuwa Gari hilo baada ya kuwagonga watembea kwa miguu lilipinduka na kisha
kutumbukia mtaloni. Aidha katika ajali hiyo watu watatu walijeruhiwa akiwemo
dereva wa Gari hilo na watu wengine wawili ambao walikuwa katika gari hilo
ambao ni ALLAN JAMES ALLAN [30]
Mkazi wa Bagamoyo na NKUNDWE JOEL
KASOKELA [29] Mkazi wa Msasani.
Chanzo
cha ajali kinachunguzwa. Majeruhi wamehamishiwa Hospitali ya Rufaa Mbeya kwa
matibabu zaidi. Mtuhumiwa ambaye ni dereva wa gari hiyo amekamatwa na amelazwa
Hospitali ya Wilaya ya Rungwe - Makandana akiwa chini ya ulinzi wa Polisi.
Miili ya marehemu imehifadhiwa Hospitali ya Wilaya ya Rungwe - Makandana.
Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya
limeendelea kukabiliana na matukio makubwa ya uhalifu pamoja na wahalifu. Jitihada
zinaendelea kwa kushirikiana na wananchi kuhakikisha Mkoa wetu unakuwa mahala
salama. Hata hivyo Kumekuwa na matukio 02 ya mauaji kama ifuatavyo:-
Mnamo tarehe 22.10.2017 majira ya saa
13:00 mchana huko Kijijj cha Mwala, Kata ya Ilembo, Tarafa ya Isangati,
Wilaya ya Mbeya Vijijini, Mkoa wa Mbeya, Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la ASA MWILE @ MWASENGA [21] Mkazi wa Kijiji
cha Masoko aliuawa kwa kupigwa na kundi la wananchi walioamua kujichukulia
sheria mkoanani wakitumia silaha za jadi fimbo na mawe.
Inadaiwa
kuwa chanzo cha tukio hilo ni tuhuma za wizi baada ya marehemu kukutwa akivunja
duka mali ya ZICKY YORAM [34] Mkazi
wa Mwala hivyo wananchi kupiga yowe na kuanza kumshambulia hadi kufa. Mwili wa
marehemu umehifadhiwa Hospitali Teule ya Ifisi. Upelelezi unaendelea
Mnamo tarehe 22.10.2017 majira ya saa
07:00 asubuhi huko maeneo ya Sae, Kata ya Ilomba, Tarafa ya Iyunga, Jiji na
Mkoa wa Mbeya. Mtu asiyefahamika jina
wala anuani yake mwenye jinsia ya kiume anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka
20-30 jinsia ya kiume aliuawa kutokana na kupigwa na wananchi wanaojichukulia
sheria mkononi.
Chanzo
cha tukio ni tuhuma za wizi. Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Rufaa
Mbeya. Watuhumiwa wanne wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo na mahojiano zaidi
yanaendelea. Upelelezi unaendelea.
WITO:
Kaimu
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishina Msaidizi wa Polisi MUSSA A. TAIBU anatoa wito kwa Madereva
kuwa makini wanapotumia vyombo ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika. Kaimu Kamanda
TAIBU anawataka madereva kufuata, kuheshimu
na kuzingatia sheria na alama za barabarani ili kuepuka ajali. Aidha anatoa
wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi ikiwa ni
pamoja na kutoa taarifa za uhali/wahalifu na watuhumiwa mbalimbali wa uhalifu
ili wachukuliwe hatua stahiki za kisheria. Pia Kamanda TAIBU anawataka wananchi kutii sheria bila shuruti na kuacha
kujichukulia sheria mkononi kwani ni kinyume cha sheria na kamwe Jeshi la
Polisi halitakuwa na huruma na mtu yeyote wala kikundi cha watu watakaoshindwa
kutii sheria.
Imesainiwa na:
[MUSSA A. TAIBU - ACP]
KAIMU KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA
No comments:
Post a Comment