MKURUGENZI WA SHULE YA MWIGO AKITOA SHUKRANI
KAKA MKUU AKIPOKEA VITABU
DADA MKUU
WANAFUNZI WA MWIGO SEKONDARI
WAKUU WA SEKONDARI WILAYANI KYELA WAMEIPONGEZA READ
INTERNATIONAL KWA MSAADA WA VITABU
shirika la Read International kutoka nchini uingereza wakishirikiana na wakurugenzi
wa kyela fm radio wameweza kutoa msaada wa vitabu vya ziada kwa masomo yote yafundishwayo kwenye shule za sekondari wilayani ili kuinua
kiwango cha elimu
Msaada huo ulianza
kutolewa jana kwa shule ya
sekondari Mwigo ambapo waliweza kutoa jumla ya vitabu 324
pamoja na sekondari Ikimba ambayo
ilipatiwa jumla ya vitabu 210 ambapo leo ukiwa ni muendelezo wa zoezi hilo
chini ya mwakilishi wao ambaye ni acting manager Billy George wameweza kutoa
tena msaada wa vitabu 324 kwa shule ya sekondari Ikolo
Ambapo kaimu mkuu wa
shule hiyo Robert Mwakafwila ameweza kupokea msaada huo wa vitabu kutoka kwa
wahisani hao na kuwaahidi kuwa watavitunza vitabu hivyo na kuweza kuwa
patia maarifawanafunzi wao nakubwa
zaidi ni kuwahamasisha wanafunzihao kusoma kwa hari na bidii pia
kwa upande wake kiranja mkuu wa sekondari ya Ikolo Lucas
Erasto amewapongeza wahisani hao kwa vitabu walivyowapatia kuahidi kuwa msaada
huo usiwe mwisho bali uwe endelevu kutokana na changamoto ambazo zinakabili
shule zilizonyingiza sekondari wilayani
hapo kubwa ikiwa ni uhaba wa walimu wa masomo ya sayansi pamoja na hesabu
hata hivyo wahisani hao bado wanazoezi zito la kuendelea kugawa vitabu kwa sekondari nyingine
zilizobaki wilayani hapa ikiwa ni pamoja na Ipinda sekondari ambapo zoezi hilo
linatarajiwa kumalizika mwishoni mwa mwezi huu wa septemba
No comments:
Post a Comment