Tuesday, 24 September 2013

SHULE NANE WILAYANI KYELA ZAPEWA MSAADA WA VITABU




Shirika la Read International kwa kushirikiana na Wakurugenzi wa Kyela fm Radio hatimaye limekamilisha zoezi la kugawa vitabu kwa shule saba ndani ya wilaya ya kyela na moja katika wilaya ya Rungwe.
Ugawaji huo wa vitabu    ulianza tarehe kumi na tisa nakukamilika tarehe ishirini na nne{24/09/2013}.shule zilizo pata msaada huo ni Mwigo,Ikolo,Ikimba,Ngana,Ipinda,Mwaya,Kayuki na Bujonde.
Akizungumzia msaada huo Meneja msaidizi wa kyela fm radio ndugu Billy Mwaigoga alisema vitabi hivyo vilivyo tolewa na Read international ni vya ziada na wala si vya kiada,hivyo vitaongeza uelewa wa mwanafunzi endapo wata vitumia vizuri,pia amewaasa wanafunzi kuwa na tabia ya kupenda kusoma na kuacha tabia utoro wakati wa masomo
 Kaimu mkuu wa shule ya ikolo ndugu Robert Mwakafwila amewashukuru sana Wakurugenzi wa Kyela fm radio kwa kuwa na moyo wa kupenda kusaidia jamii ya watanzania nakuwataka wasiishie hapo bali waendelee kuwasaidia.
kwa upande wake kilanja mkuu wa sekondari ya Ikolo Lucas Erasto amewapongeza wahisani hao kwa vitabu walivyowapatia kuahidi kuwa msaada huo usiwe mwisho bali uwe endelevu kutokana na changamoto ambazo zinakabili shule zilizonyingiza sekondari  wilayani hapo kubwa ikiwa ni uhaba wa walimu wa masomo ya sayansi pamoja na hesabu
Wanafunzi wa Ngana Sekondari wame shukuru sana na kusema sasa kilio chao cha muda mrefu cha upungufu wa vitabu vya kujisomea kimesikilizwa na pia wameomba wakurugenzi wa kyela fm radio kusaidia na upande wa michezo mashuleni.
Afisa mtendaji wa Kata ya Ipinda ndugu Carthbert Mwalukama  naye alitoa shukrani zake kwa Read international kwa kushirikiana na Wakurugenzi wa Kyela fm Redio kwa msaada huo wa Vitabu katika shule ya Ipinda sekondari pia alisema Wakurugenzi wa kyela fm wamekuwa ni msaada mkubwa kwa shule hiyo ni baada ya hapo awali kutoa msaada wa Mabati mia moja kwa ajili ya vyumba ya madarasa.
wananchi wameiomba serikali kwa kushirikiana na wahisani mbalimbali kuendelea kuzisaidia Shule ambazo  zimekuwa na ukosefu wa vitabu vya kiada na ziada

No comments: