Na : James Mwakyembe
Mtu mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Joshua Paul (31) mkazi
wa kijiji cha Ntokela wilayani Rungwe ameuawa na watu wasiofahamika na kutupwa
kwenye shamba la mahindi jana jioni.
Akifafanua zaidi kuhusu tukio hilo kamanda wa polisi wa mkoa
wa Mbeya, kamishina mwandamizi wa jeshi la polisi Ahmed Z. Msangi amesema, mwili wa
marehemu ulikutwa kwenye shamba la mahindi linalomilikiwa na bwana Yohana
Mbilinyi, ukiwa umekatwa kitu chenye ncha kali sehemu ya paji la uso na
kifuani.
Bwana Msangi ameongeza kuwa tayari polisi wanamshikiria
Belisi Sikakinda (28) mkazi wa kijiji cha Kiwira wilayani Rungwe, ambaye alikuwa
na marehemu siku ya mwisho, huku uchunguzi zaidi kuhusu tukio hilo ukiendelea
kufanyika.
Kamanda Msangi ametoa wito kwa jamii kushirikiana na jeshi
la polisi ili kuwabaini wahusika wa mauaji hayo na sheria ichukue mkondo dhidi
yao.
No comments:
Post a Comment