Wednesday 30 April 2014

‘Shilingi 2,000 ziliniponza nikaibiwa mtoto’

boka 7a13d

Aprili 6, mwaka huu ni siku ambayo mkazi wa Kijiji cha Kibanda wilayani Kyela, Mboka Mwakikagile (20) haitaisahau.
Ni siku ambayo aliibiwa mtoto mchanga wa kiume aliyekuwa na umri wa siku saba tu.
Akisimulia tukio hilo, Mboka anasema alijifungua salama Machi 30 akiwa nyumbani kwa wazazi wake ambao ni Lupalo Mwakikagile (90) na mkewe Nelly Kyusa (49).
Anasema akiwa katika siku ya saba, alipigiwa simu na mzazi mwenzake (jina linahifadhiwa) kwamba mama yake mkubwa atafika nyumbani kumwona mtoto.
Anasema baada muda mfupi mwanamke huyo alifika kwa pikipiki akiwa na mkoba uliokuwa na nguo za mtoto, sabuni na vifaa vingine. "Baada ya kumkaribisha na kusalimiana na wote , mwanamke huyo alimchukua mtoto na baadaye alinishauri twende Zahanati ya Njisi akatibiwe jicho ambalo lilikuwa linamsumbua kidogo,''anasema.
Mboka na mwanamke huyo waliondoka kwenda kwenye zahanati hiyo kwa pikipiki na kwamba baada ya kufika hapo, daktari aliwataka wanunue daftari na mwanamke huyo alitoa Sh2,000 na kumtaka akanunue.
''Nilipokea fedha hizo na kumwachia mtoto pamoja na simu yangu wakati mimi nikielekea kununua daftari kwenye duka lililo mbali na zahanati hiyo,'' anasema.
Anasema mara baada ya kurudi dukani alishtuka kutomwona mwanamke na mtoto wake.'Kitendo hicho kilinishtua zaidi kwani mzazi mwenzangu aliondoka bila ya kunishirikisha kwamba tukaripoti polisi na kibaya zaidi yeye ndiye aliyedai kwamba ni mama yake mkubwa,'' anasema

No comments: