Friday 6 June 2014

WANAFUNZI WA CHUO CHA HABARI DIGITAL MEDIA COLLEGE OF TANZANIA[DMCT] WACHANGIA DAMU KATIKA KITENGO CHA DAMU SALAMA











      Miongoni mwa Wanafunzi wa DMCT waki fanya mahojiano ndugu Baraka Thomas wa Kitengo cha Damu salama

Na; JOSHUA CHUWA,MWASHA FASTON
          Benki ya damu salama nyanda za juu kusini wametembelea katika chuo cha habari digital media college of Tanzania kilichopo jijini mbeya katika eneo la nanenane,lengo ikiwa nikutoa elimu juu ya uchangiaji wa damu salama ili iweze kuwasaidia wagojwa waliopo hospitalini hususani wakina mama wajawazito na watu wanaofanyiwa upasuaji.
        Akizungumza na wanafunzi wa dmct Ndugu Baraka Thomas Masanja alieleza kuwa wanajamii wanapaswa kujitolea  kuchangia damu ili iweze kusaidia wagojwa mbalimbali wenye matatizo tofauti kama wakina mama wajawazito, majeruhi ,wagojwa wa muda mrefu ,na wagojwa  wanaofanyiwa upasuaji katika hospitali mbalimbali hapa nchini.
      Sanjari na hayo  Baraka alisema kuwa jamii inapaswa kuelewa kuwa damu iliyopo mahospitalini  haiuzwi na benki ya damu hainunui damu endapo mgojwa akiuziwa damu anatakiwa kutoa taarifa katika ofisi za benki ya damu salama au kuwasiliana na ofisi za damu salama kwa namba  0757107676.
     Wakizungumza na Mtandao huu Wanafunzi wa Digital Media College of Tanzania [DMCT]wamesema wameamua kuchangia Damu kwa lengo la kusaidia na kuokoa Maisha ya wenye uhitaji wa Damu.
Miongoni mwa Wanafunzi waliochangia Damu ni Raisi wa Chuo anaye julikana kwa jina la James Mwakyembe,Makamu wa Raisi wa Chuo Betrida Mwasambalila na Waziri wa Mahusiano ya Nnje Ndugu Bahati Msilu.

No comments: