Wednesday 4 June 2014

UZINDUZI WA LIGI YA MPIRA WA MIGUU PAMBANA SAIDIA JAMII KYELA



                            Mjezaji wa timu ya Vijana Ikolo Emmanuel Mwagamwaga

       Mkurugenzi wa Asasi ya PAMBANA SAIDIA JAMII

Hatimae ligi ya mpira wa miguu maarufu kama Pambana Saidia jamii imezinduliwa rasmi huko wilayani kyela,
akizungumza na mtandao huu Mwenyekiti mtendaji wa Asasi ya Pambana saidia jamii Ndugu Abraham Mwanyamaki amesema kuwa wameamua kudhamini ligi hiyo kwa lengo la kuibua vipaji ndani ya Wilaya ya kyela.
katika uzinduzi huo kulifanyika mchezo wa Ngao ya Hisani kati ya Bingwa mtetezi ambayo ni Vijana Ikolo na Small Boys  na Vijana ikolo kuibuka mshindi kwa kuifunga Small Boys Gori mbili kwa moja na kuondoka na kitita cha Tsh 100000 na Small Boys kujipatia Tsh 50000.
Pia mwenyekiti alisema kuwa katika mashindano hayo Mshindi wa kwanza atajipatia kiasi cha Tsh 500000 na kombe lenye dhamani ya Tsh 200000 wakati mshindi wa pili ataibuka na Tsh 300000,wa tatu Tsh 200000 na wanne 100000.
Wakiti huohuo Mfungaji Bora atajinyakulia Tsh 40000,Mchezaji Bora Tsh 40000,Timu bora Tsh 50000 na Mwamuzi Bora Tsh 30000

No comments: