Thursday 29 May 2014

ASASI YA PAMBANA SAIDIA JAMII YAWA MKOMBOZI KWA WANANCHI WA KYELA

                                                   Mkurugenzi wa asasi ya pambana saidia jamii
                                     kiongozi wa mbio za mwenge bi Recho kasanda





Asasi ya pambana saidia jamii iliyopo wilayani kyela chini ya mwenyekiti mtendaji ndugu Abraham Mwanyamaki leo wamefanya uzinduzi wa mradi wa uzalishaji wa nishati ya gesi hai{Biogas} ambao umezinduliwa na kiongozi wa mbio za Mwenge Ndugu Rachel Steven Kassanda katika kijiji cha kasumulu, mradi huo umeghalimu kiasi cha Tsh 2,700,000.
Akiongea na mtandao huu mwenyekiti mtendaji amesema kuwa mradi huwa wa gesi asilia unatekelezwa katika tarafa mbili mbili za wilaya ya kyela ambazo ni tarafa ya Ntebela na tarafa ya unyakyusa.
Pia ametoa wito kwa wananchi wa wilaya ya kyela kuendelea kuunga mkono shughuri zinazofanywa na asasi katika kuleta maendeleo ndani ya wilaya ya kyela

No comments: