Friday, 24 April 2015

David Petraeus alitoa siri za Jeshi


Mkuu wa zamani wa Shirika la kijasusi nchini Marekani, David Patraeus
Jaji wa mahakama ya jimbo la North Carolina nchini Marekani amemhukumu mkurugenzi wa zamani wa shirika la kijasusi la CIA, Jenerali David Petraeus kwa makosa ya kutoa siri za kijeshi kwa mpenzi wake.
Patraeus ametakiwa kulipa fine ya dola za kimarekani lakimoja.
Awali Jenerali huyo alikana kufanya makosa hayo lakini baadae alikiri kutoa taarifa hizo kwa mpenziwe Paula Broadwell ambaye alikuwa na uhusiano nae wa kimapenzi alipokuwa Mkuu wa CIA.
Mwandishi wa BBC jijini Washington amesema kuwa inaaminika kuwa Petraeus ataendelea na kazi yake ya sasa ya Mshauri wa maswala ya usalama Ikulu

No comments: