Dar es
Salaam, Aprili 16, 2015 –
Mtandao wa Wanawake
na Katiba Tanzania unaounganisha wanawake kutoka asasi za kiraia za nyanja mbali
mbali za kisiasa, kijamii na kiuchumi, unatambua jitihada zote zilizofanywa na
zinazoendelea kufanywa katika kuhakikisha kwamba Katiba Mpya ya Tanzania inajengwa
katika misingi ya usawa wa jinsia. Kwa mtazamo wa Mtandao,
Katiba Pendekezwa
imejengwa katika misingi inayotambua ulinzi
wa utu, heshima na haki za wanawake na hivyo
inahitaji kuthaminiwa na kulindwa na wahusika mbalimbali, wakiwemo viongozi wa
vyama vya siasa nchini.
Kwa mantiki
hiyo ya kuhakikisha kwamba yaliyomo katika Katiba pendekezwa yanalindwa,
Mtandao wa Wanawake na Katiba umekua ukifuatilia kwa makini mwenendo wa viongozi,
na haswa viongozi wa vyama vya kisiasa katika matamko yao mbalimbali wanayoyatoa,
yakiwemo yale yanayohusu mapendekezo ya kubadilisha sheria ya uchaguzi.
Kwa mfano,
viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa wamekuwa wakiikumbusha serikali kuzingatia
katika mabadiliko ya Sheria mpya ya Uchaguzi, madai matano yakiwemo: Ushindi wa
Mgombea Urais uwe wa kura za asilimia hamsini na zaidi, Nafasi ya Mgombea
Binafsi itambuliwe, Tume Huru ya Uchaguzi iwepo na uwezekano wa kupinga matokeo
ya uraisi mahakamani.
Hata hivyo,
matamko haya hayajumuishi kuingizwa kwa msingi wa usawa wa jinsia katika mabadilko
ya Sheria yanayopendekezwa, pamoja na michakato mingine mbalimbali ya uchaguzi
na matokeo yake.
Mwenendo huu wa viongozi wa Vyama vya Siasa unatushangaza na
kutuonyesha kuwa viongozi wengi wa kisiasa hawatilii maanani ajenda ya kuleta
usawa wa jinsia katika uongozi wa nchi hii. Kwa maana hiyo, viongozi hawa
wanaashiria kutotambua mchango, nguvu, nafasi
na haki wa mwanamke katika nyanja hii muhimu na hivyo kuduwazaa demokrasia na
maendeleo ya nchi hii kwa ujumla.
Mtandao wa
Wanawake na Katiba unawakumbusha na kuwataka viongozi hawa kutambua kwamba:
·
Wanawake
ni Zaidi ya asilimia 51% ya raia wa Tanzania ambao utawala wa nchi unawahusu.
·
Wengi
wa wanachama wao ni wanawake, na hivyo wana nafasi kubwa ya kushawishi wananchi
kutounga mkono itikadi, sera na mwenendo wa vyama vyao vya kisiasa;wanawake
tumechoka kutumika na vyama vya siasa kama wapiga debe; wahamasishaji wa
michangi ya vyama;
·
Wanawake
ni idadi kubwa ya wapiga kura pamoja na watunzaji wakuu wa familia na amani ya
nchi hii;
·
Vyama
vya kisiasa visivyozingatia usawa wa jinsia na hivyo kuchochea sera za kibaguzi
havina nafasi katika ujenzi wa taifa letu haswa kufuatia kukomaa kwa harakati
za jinsia nchini
Hivyo basi,
tunatoa rai kuwataka viongozi wa vyama vya kisiasa kuhakikisha wanazingatia
yaliyomo katika Katiba pendekezwa na kuendelea kuyatetea huku wakihakikisha
kwamba matamshi na sera za kibaguzi hazitavumuliwa.
# # #
Kama
ungependa habari zaidi kuhusu mada hii, tafadhali wasiliana na TGNP ambao ni
mojawapo wa wanachama wa mtandao kupitia +255754784050.
|
No comments:
Post a Comment