Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Bi MBONI MHITA akizungumza mbele ya wakazi wa kijiji cha Sawala wilayani Mufindi (hawapo pichani),wakati akizindua chanjo kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka 5 kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Iringa.
Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Bi MBONI MHITA akiwa amembeba mtoto mara baada ya kumpa chanjo.
wakazi wa kijiji cha Sawala wilayani Mufindi wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Bi Mboni Mhita,mara baada ya kuzindua chanjo kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka 5 kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Iringa.
Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Bi MBONI MHITA akimpa chanjo mmoja wa watoto katika kijiji cha Sawala wilayani Mufindi mkoani Iringa
Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Bi MBONI MHITA amewataka wazazi na walezi Mkoani Iringa kutosikiliza maneno ya uzushi kuwa chanjo zinazotolewa kwa Watoto nchini huwa zinamadhara, badala yake wajitokeze kwa wingi kwenye vituo vya kutolea chanjo ili kuwakinga watoto na uwezekano wa kushambuliwa na maradhi mbali mbali.
Taarifa ya ofisi ya habari na mawasiliano ya halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, imeeleza kuwa ,Mkuu wa wilaya aliyasema hayo katika kijiji cha Sawala Wilayani Mufindi Mkoani iringa wakati akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwenye uzinduzi wa wiki ya chanjo kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka 5.
Mhita amesema endapo wazazi na walezi watasikiliza maneno yasiyo na ukweli wowote, watakuwa wanahatarisha afya za watoto wao kwani kuzikosa chanjo hizo muhimu kwa ustawi wa Mtoto kutasababisha washambuliwe na maradhi, kitu ambacho kinahatarisha uhai wa Mtoto.
Amesema chanjo ni mkakati muhimu na muafaka katika kutokomeza maradhi na kupunguza vifo vya watoto lakini pia kupunguza gharama kubwa ambazo Familia na taifa kwa ujumla lingetumia katika kutibu maradhi yatokanayo na magonjwa yanayozuilika kwa chanjo.
Wataalam ya afya wamethibitisha kuwa, chanjo huzuia takribani vifo milioni mbili hadi tatu kila mwaka kutokana na maradhi yanayokigwa kwa chanjo ikiwa ni pamaoja na Ndui, Polio, Kifaduro na Pepopunda,ujumbe wa chanjo mwaka huu unasema Jamii iliyochanjwa ni jamii yenye afya huku kauli mbiu ikisema Chanjo ni zawadi ya Maisha
No comments:
Post a Comment