Saturday, 25 April 2015

WAKULIMA NA WAFUGAJI WAMUOMBA WAZIRI KUINGILIA KATI MGOGORO WA ARDHI


Wakulima na wafugaji zaidi ya 3000 wa vijiji vya Madanga na Jaira wilayani pangani wamemuomba waziri wa ardhi,nyumba na maendeleo ya makazi kuingilia kati mgogoro wa ardhi uliosababisha wananchi hao kunyang'anywa mashamba yao kisha kupewa mwekezaji hatua ambayo inaweza kusababisha machafuko baina ya pande hizo mbili.
Wakizungumza baada ya mkuu wa wilaya ya pangani Bi,Regina Chonjo pamoja na kamati yake ya ulinzi na usalama alipokwenda katika kijiji cha Madanga kutoa maamuzi kuhusu mgogoro huo kisha kuwapa eneo hilo lenye ukubwa wa hekari 300 wawekezaji wa taasisi mojawapo ya dini,viongozi wa wakulima hao wamesema hawatakubali kuachia mashamba yao hadi waziri mwenye dhamana atakapoingilia kati.
Kwa upande wake mratibu wa wafugaji wa kijiji cha Jaira Bwana. Chambega Muhaka Chambega amesema endapo suala hilo halitatafutiwa ufumbuzi wa kina haraka iwezekanavyo wakulima watakosa eneo la kilimo katika msimu ujao wa kilimo kwa sababu viongozi wa halmashauri wanalifumbia macho suala hilo kwa sababu lilitolewa kama zawadi kwa taasisis hiyo na mkuu wa wilaya mstaafu Margareth Ndaga hatua ambayo inaweza kusababisha umwagaji damu.
Kufuatia hatua hiyo mkuu wa wilaya ya Pangani Bi,Chonjo amesema hatua alizochukua kuwapatia wawekezaji eneo hilo zinatokana na vielelezo ambavyo taasisi ya dini ya kanisa anglikana imewasilisha kwa afisa ardhi hivyo amewashauri wakulima na wafugaji kuwa endapo hawajaridhika na hatua hiyo ni vyema wakafuata utaratibu wa kisheria ikiwa ni pamoja na kwenda baraza la ardhi kisha baadae mahakamani

No comments: