Wednesday, 15 April 2015

Wahamiaji haramu waaga dunia katika pwani ya Libya

Wahamiaji haramu waaga dunia katika pwani ya Libya


Wahamiaji haramu zaidi ya 400 wameaga dunia katika pwani ya Libyabaada ya boti waliyokuwa wakisafria kuzama jana katika pwani hiyo.

 Askari wanaolinda pwani ya Italia awali walisema kuwa wamefanikiwa kuwaokoa wahamiaji haramu 144 na kupata miili kumi ya wahamiaji haramu waliozama na kisha kuipeleka hadi pwani.

 Shirika la habari la Ufaransa limeripoti kuwa, wahamiaji hao haramu waliozama ambao  wengi wao walikuwa ni kutoka nchi za Kiafrika na za eneo la Mashariki ya Kati walikuwa na lengo la kuingia Italia kinyume cha sheria kupitia Libya.

 Miezi kadhaa iliyopita pia, mamia ya wahamiaji haramu kutoka nchi za Kiafrika waliaga dunia wakiwa katika maji ya bahari ya Mediterania wakisafari kuelekea nchi za Ulaya.   

No comments: